Friday, January 27, 2012

Mameneja TANROADS Mikoani Wabadilishwa

Mtendaji Mkuu wa Tanroads Eng. Patrick Mfugale amefanya mabadiliko makubwa kwenye safu ya uongozi ya Tanroads katika mikoa yote 25 ya Tanzania Bara.

Mabadiliko haya yamelenga kuongeza ufanisi katika kusimamia miradi ya barabara hasa huko mikoani na kwamba Mameneja hao wa mikoa sasa watawajibika kusimamia ubora wa kazi, kukamilika kwa miradi hasa ya maendeleo ndani ya muda wa mkataba hasa kwa miradi inayohusu mikoa yao na kuhakikisha kuwa thamani ya fedha zilizotumika ‘value for money’ inazingatiwa. Katika mabadiko hayo kuna Mameneja saba wapya. Mameneja wengine watano wamehamishwa vituo, Mameneja wanne wakiteuliwa katika mikoa mipya na Mameneja tisa wakiwa wamebaki katika vituo vyao vya zamani.

Mameneja saba wapya walioingizwa katika mabadiliko haya ni:

Mkoa wa Dar es Salaam , Eng. Julius Ndyamukama ambaye alikuwa Tanroads Makao Makuu na amechukua nafasi ya James Nyabakari aliyehamishiwa Mbeya ambako Eng. Lucian Kileo aliyekuwa huko amehamishiwa Tanroads Makao Makuu ambako atapangiwa kazi nyingine.

Mkoa wa Kilimanjaro ameteuliwa Eng. Mwita Marwa Rubirya akitokea Wizara ya Ujenzi Makao Makuu. Naye Eng. Tumaini Sarakikya aliyekuwa Meneja wa mkoa huo amehamishiwa mkoa wa Pwani.

Eng. Isaac Mwanawima amehamishiwa mkoa wa Lindi akitokea Makao Makuu ya Wizara ya Ujenzi akichukua nafasi ya Eng. Michael Kulaya anayehamia Tanroads Makao Makuu.

Eng. Dorothy Mtenga amepelekwa Morogoro akitokea Tanroads Dodoma na anachukua nafasi ya Eng. Charles Madinda ambaye sasa amehamishiwa Tanroads Makao Makuu. Huko Shinyanga Eng. Augustine Witonde Philip amepangiwa mkoa huo akitokea Tanroads Dar es Salaam , anachukua nafasi ya Damian Ndabalinze ambaye amehamishiwa mkoa wa Tabora.

Kwa Mkoa wa Rukwa amehamishiwa Eng. Florian Kabaka ambaye awali alikuwa Tanroads Makao Makuu na anachukua nafasi ya Eng. Joseph Nyamhanga ambaye ameteuliwa kukaimu nafasi ya Mkurugenzi wa Barabara, Wizara ya Ujenzi. Nafasi hiyo ya Mkurugenzi wa Barabara ilikuwa wazi kufuatia kuteuliwa kwa Eng. Mussa Iyombe kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Aidha Eng. Isaack Kamwelwe amehamishiwa mkoa mpya wa Katavi akitokea Wizara ya Ujenzi Makao Makuu.

Mameneja watano waliohamishiwa mikoa mingine ni:

Eng. Damian Ndabalinze anahamia Tabora akitokea Shinyanga. Hapa Eng. Ndabalizne amechukua nafasi ya Eng. Partson Masebo aliyehamishiwa Makao Makuu ya Tanroads. Eng. Tumaini Sarakikya maepelekwa mkoa wa Pwani akitokea mkoa wa Kiliamnjaro. Aliyekuwa Meneja wa Tanroads mkoa wa Pwani Eng. Gabriel Mwikola amepelekwa Mtwara ambapo Eng. Mussa Mataka aliyekuwa Meneja wa mkoa huo amepangiwa Tanroads Makao Makuu. Naye Eng. James Nyabakari amepelekwa Mbeya akitokea Dar es Salaam.

Mameneja wanne waliopangiwa mikoa mipya kama ifuatavyo:

Eng. Haruna Senkuku anakwenda mkoa wa Geita akitokea mkoa wa Kigoma. Nafasi yake kwa mkoa wa Kigoma inafanyiwa kazi.

Mkoa wa Katavi amepelekwa Eng. Isaack Kamwelwe ambaye awali alikuwa makao makuu Wizara ya Ujenzi. Kwa mkoa wa Njombe Eng. Yusuf Mazana ameshika nafasi ya Meneja wa Mkoa akitokea ofisi ya Tanroads mkoa wa Ruvuma . Mkoa wa Simiyu amepelekwa Eng. Emanuel Kibeya ambaye ametokea ofisi ya Tanroads mkoa wa Tabora.

Mameneja tisa waliobaki katika vituo vyao vya zamani ni kama wafuatavyo;

Mkoa wa Arusha – Eng. Deusdedit Kakoko, Mkoa wa Dodoma – Eng. Leonard Chimagu, Mkoa wa Iringa – Eng. Poul Lyakurwa, Mkoa wa Kagera - Eng. Johnny Kalupate, Mkoa wa Mara – Eng. Emmanuel Korosso, Mkoa wa Manyara - Eng. Yohani Kasaini, Mkoa wa Mwanza – Eng. Leonard Kadashi, Singida – Eng. Yustaki Kangole na Mkoa wa Tanga amebakia Eng. Alfred Ndumaro.

Taarifa hii imetolewa na;

Martin Ntemo

Msemaji wa Wizara ya Ujenzi.

1 comment:

  1. Hotel Review - Casinos Near the Casino - Georgia - Goyang
    Best Hotel Near the 1xbet korean Casino If 포커 게임 you are visiting Georgia, we will be in the area. This casino offers 스코어 사이트 a full range of entertainment 1xbetmobi and 야구 사이트

    ReplyDelete